Monday, 4 September 2017

SASA SIMBA, YANGA KUKIWASHA CHAMAZI

Baada ya danadana ya muda mrefu hatimaye Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limeamua michezo ya Simba na Yanga ambayo itahusisha Azam FC itachezea kwenye Uwanja wa Azam Complex maarufu kwa jina la Uwanja wa Chamazi.
Maamuzi hayo ni yale ya kuiwezesha Azam FC kuwa nyumbani baada ya awali timu hiyo kutopewa haki ya kucheza uwanja wa nyumbani kutokana na kilichodaiwa kuwanja wao kuwa mdogo na hivyo kutokidhi mahitaji ya kucheza dhidi ya Simba na Yanga uwanjani hapo.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa ili kuipa Azam FC haki yake katika kuutumia uwanja huo ambao unachukua idadi ya mashabiki 7,000 waliokaa kwenye siti.
Amesema kuwa kitakachofanyika ni kuwa tiketi zitakazouzwa ni zitakazotosha kwa idadi ya siti na hazitauzwa zaidi ya idadi halisi ya siti zilizopo uwanjani, hivyo wale watakaokosa watatakiwa kutosogea uwanjani kwa kuwa ulinzi utakuwa mkubwa.
Mchezo ujao wa Azam FC na Simba utakaochezwa uwanjani hapo, utachezwa saa moja usiku ili kupisha mchezo wa mapema wa  siku hiyo katika Ligi Kuu Bara kati ya Prisons na Majimaji utakaochezwa saa kumi jioni.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive