Wednesday, 13 September 2017

MKUDE AANDALIWA, JUMAPILI KAZI IPO

Kikosi cha Simba kimeendelea na mazoezi ya kufa mtu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Jumatano kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya Jumapili na Mwadui FC.
Kocha wa Simba, Joseph Omog ameonekana kumwandaa Jonas Mkude kwa ajili ya kuanza kikosi cha kwanza ili kuhakikisha kikosi hicho kinaondoka na  pointi tatu.
Simba inapambana kurekebisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi yao ya wikiendi iliyopita baada ya kutoka suluhu ya 0-0 na Azam FC.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive