Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole ameshangazwa na raia wa Namibia kwa kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John P Magufuli kila sehemu nchini humo huku akisema kuwa ni sifa kwa taifa letu.
Polepole ambaye yupo nchini Namibia kikazi kwa mujibu wa maelezo yake amesema kila mtu anayekutana nae nchini humo anamuulizia Rais Magufuli.
“Niko Namibia kwa kazi ya CCM na kila mtu anamuulizia Magufuli, Magufuli, Magufuli. Huyu Magufuli amerudisha maradufu heshima ya Taifa letu”,ameandika Polepole kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Humphrey Polepole ni moja ya viongozi wa CCM ambao wanasiasa wengi wanadai kuwa nafasi aliyopewa kwenye chama hicho ni kubwa kulinganisha na uwezo wake akiwemo Mbunge wa Iringa mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
0 comments:
Post a Comment