Rekodi zinaonyesha kwamba Taifa Stars ina ukuta usiopitika kirahisi. Timu hiyo iliifunga Botswana kwa mabao 2-0 jana Jumamosi na kuwa na rekodi ya kuruhusu bao moja tu katika mechi nne zilizopita.
Katika mechi hizo, Stars ilipata suluhu na Lesotho katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu wa mashindano ya Cosafa kabla ya baadaye kupata ushindi wa penalti.
Baada ya hapo Stars ilicheza na Rwanda katika mechi ya kufuzu CHAN na kupata sare ya bao 1-1 jijini Mwanza kabla ya kupata suluhu katika mechi ya marudiano mjini Kigali.
Stars ilithibitisha kuwa ukuta wake uko vizuri baada ya jana kutoruhusu bao dhidi ya Botswana.
"Nilianza kwa kuijenga timu kuanzia kwenye ulinzi kwenda mbele, nadhani sasa tunakwenda vizuri. Timu inafanya vizuri katika ulinzi," alisema kocha wa Taifa Stars, Salum Mayanga.
0 comments:
Post a Comment