Zipo list kibao za viongozi wa dini
ambazo huonesha namna gani wanakuwa na ushawishi wa kuponya watu kiroho
lakini fahamu pia kuwa zipo list za viongozi hao hao wa dini ambao
wanatajwa kuwa na fedha nyingi zaidi duniani…na kwa mwaka huu wa 2017
tayari ninayo list ya wachungaji 10 wanaotajwa kuwa na fedha nyingi
zaidi duniani.
10. Joseph Prince Dola Milioni 5
Ni Mchungaji kutoka Singapore ambaye anatajwa kuwa na utajiri wa Dola
za Kimarekani Milioni 5. Mchungaji Joseph hufanya ibada ambazo pia
hurushwa LIVE kwenye mtandao wa youtube hivyo kupata umaarufu mkubwa sana barani Asia na duniani.
9. T.B Joshua – Dola Milioni 10
Ni mzaliwa wa Nigeria na anatajwa kuwa na utajiri wa Dola za
Kimarekani Milioni 10. Kwa Nigeria, mchungaji huyu ni maarufu kama Nabii
na ana watu wanaomfuatilia kwenye mtandao wa Facebook zaidi ya Milioni
1.5
8. Billy Graham – Dola Milioni 25
Huyu ni mchungaji wa Marekani na moja kati ya wachungaji wenye umri
mkubwa. Alizaliwa mwaka 1918 na kusomea masomo Anthropolojia na Biblia.
Anaripotiwa kuwa na waumini wanaomfuatilia zaidi ya Bilioni 2.2 na
utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 25.
7. Kenneth Copeland – Dola Milioni 25
Anafahamika sana kwa ujumbe mkubwa wa mahubiri yake ambayo ni
mafanikio na utoshelevu. Kabla ya kuwa Mkristo alikua mwanamuziki kazi
iliyompa mafanikio makubwa. Moja ya nyimbo zake ni pamoja na “Pledge of Love” alioufanya
mwaka 1957 na kuingia kwenye chat bora za Billboard kwa kushika namba
17. Yeye na familia yake wanaishi katika nyumba yenye gharama ya Dola
Milioni 6.3
6. Creflo Dollar – Dola Milioni 27
Ni Mchungaji wa Marekani, na kama jina lake lilivyo, Mchungai huyu
anamiliki gari ya thamani aina ya Rolls Royce, na nyumba tatu za gharama
ya Dola Milioni 2.5. Mwaka 2013 alishitakiwa kwa kosa la kumshambulia
mwanaye wa kike lakini baadaye kesi hiyo kuachwa kwa madai ya kutatua
kifamilia.
5. Enock Adeboye – Dola Milioni 39
Mchungaji huyu yuko Nigeria. Kanisa lake la Redeemed Christian Church of God lina matawi 14, 000 ndani ya Nigeria pekee na katika nchi nyingine zaidi ya 100 nje ya nchi hiyo.
4. Benny Hinn – Dola Milioni 42
Mchungaji huyu pia ni Mmarekani. Mafundisho yake ni kuhusu imani na
uponyaji. Anaripotiwa kuwahi kuchunguzwa na Serikali ya nchi hiyo kwa
kashfa za kutolipa kodi.
3. Chris Oyakhilome – Dola Milioni 50
Mchungaji Chris ni miongoni mwa wahungaji matajiri kutoka Afrika
ambaye anatokea Afrika Kusini. Tofauti na kuwa na waumini wengi kwenye
matawi ya Kanisa lake mchungaji huyu pia anamiliki matawi ya kazi za
misaada na elimu. Anamiliki vituo vitatu vya Televisheni ambavyo
vinapata waangaliaji hadi Milioni 2.5 kila siku.
2. Bishop T.D. Jakes – Dola Milioni 147
Askofu huyu anatokea Marekani na anaongoza Kanisa la Potter’s House. Amewahi kuonekana na Maraisi wa Marekani George Bush na Barack Obama ambao kwa nyakati tofauti wamemsifia mchungaji huyo kwa kuwa mwaminifu.
1. Bishop David Oyedepo – Dola Milioni 150
Huyu ndiye Mchungaji tajiri kuliko wote duniani ambaye anamiliki Kanisa lijulikanalo kama Winners Chapel. Kanisa lake ndilo Kanisa kubwa kuliko yote duniani ambalo linachukua zaidi ya waumini 50,000 kwenye ibada moja.
Kanisa lake lina matawi katika nchi 45 barani Afrika ikiwa ni pamoja na mengine nchini Dubai, Uingereza na Marekani.
0 comments:
Post a Comment