Friday, 15 September 2017

AJIBU ATIKISA MAJIMAJI

 
KIPA Ramadhan Kabwili alikuwa benchi kushangilia bao la Ibrahim Ajib dhidi ya Njombe Mji wikiendi iliyopita lakini kilochomkuta leo mazoezini hatasahau.Kabwili amejikuta kwenye wakati mgumu leo jioni baada ya kukumbana na kimbunga Ajib.
Kwenye mchezo ulipita Ajib alifunga bao la umbali mrefu kwa mpira wa adhabu kama alivyorudia leo mazoezini na kumpa wakati mgumu Kabwili aliyejiunga na Yanga msimu huu akitokea Serengeti Boys.
Pamoja na kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali kumpa Kabwili maelekezo yote ya namna ya kupangua faulo hiyo alijikuta akiambulia patupu.
Ajib ataongoza safu sa ushambuliji ya Yanga kesho dhidi ya Majimaji.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive