Licha ya kuwa winga Ramadhani Singano alikuwa akiwania na Yanga
ambapo tayari mazungumzo yalikuwa yameshafanyika ili asaini kikosini
hapo, mchezaji huyo amepiga kona na kurejea katika timu ya Azam FC.
Singano alimaliza mkataba na Azam FC mwezi uliopita, alisafiri kwenda
nchini Morocco kwa ajili ya kufanya majaribio ya kucheza soka la
kujlipwa lakini alishindwa kuafikiana na klabu iliyompeleka kwa kile
kilichoelezwa kuwa wakala wake ndiye aliyechangia kuvurugika kwa dili
hilo.
Baada ya kurejea jijini Dar es Salaam alikuwa mchezaji huru ambapo
ilifahamika kuwa Yanga ilimhitaji na tayari makubaliano yalishafikiwa
kilichobaki ni kusaini.
Awali Singano mwenyewe alisema baada ya kurejea nchini alifuatwa na
timu tatu kumshawishi asajili ambazo ni Azam FC, Singida United na
Yanga.
Akizungumzia usajili huo, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd alisema
ni kweli wamemrejesha kundini Singano na ameshasaini mkataba mpya wa
kuendelea kuichezea timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment