Klabu ya Yanga imerudisha tena mazungumzo na mshambulizi wake wa zamani, Mrisho Ngassa.
Taarifa za ndani zinaeleza Yanga imefanya mazungumzo juzi na jana usiku.
“Kama yakifikiwa makubaliano basi Ngassa anaweza kusajili siku ya mwisho ya dirisha ambayo ni leo,” kilieleza chanzo.
Awali, Ngassa alijaribu kurudi Yanga lakini zoezi hilo halikufuata utaratibu likakwama.
Lakini
kuondoka kwa Saimon Msuva, kunafanya nafasi yake ya kurejea Yanga izidi
kuongezeka na huenda muda mfupi ujao kama watakubaliana anaweza kusaini
Yanga na kurejea rasmi.
0 comments:
Post a Comment