Thursday 17 August 2017

WABUNGE WA LIPUMBA WAIISHIA MAHAKAMANI


Mahakama  Kuu imeahirisha hukumu juu ya pingamizi lililowasilishwa na wabunge nane wa Viti Maalum CUF kupinga Bunge la Tanzania kuwaapisha wabunge wapya walioteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili , Prof. Ibrahim Lipumba.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano  CUF anayeunga mkono upande wa Maalim Seif, Mbarala Maharagande, amesema mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi  Agosti 25 mwaka huu itakapotoa uamuzi kuhusu suala hilo.

Maharagande aliyasema hayo alipoongea na waandishi wa habari baada ya kutoka  nje ya mahakama hiyo.

Wabunge hao nane wa CUF(upande wa Maalim Seif) walifungua kesi kupinga kuapishwa kwa wabunge nane wanaomuunga mkono Prof Lipumba walioteuliwa baada ya wao kuvuliwa uanachama kwa tuhuma zinazowakabili za kukihujumu chama hicho kwa maelezo kuwa walitaka kushirikiana na CHADEMA kumwondoa yeye (Lipumba) madarakani.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive