Jengo la klabu ya Yanga lililopo mtaa wa Jangwani na Twiga lilipaswa
kuuzwa leo Alhamisi badala ya Jumamosi Agosti 19 kama ilivyoonyeshwa
katika tangazo lililochapishwa kwenye vyombo vya habari.
Mkurungezi
wa Msolopa Investment Company, Ibrahim Msolopa ameiomba mahakama ya
Ilala iwapangie tarehe nyingine watakayofanya mnada wa kuuza jengo la
Yanga inayodaiwa deni la Sh. 360 milioni na Wizara ya Ardhi na Maendeleo
ya Makazi.
Msolopa ni dalali wa mahakama amesema,
maombi hayo ni baada ya kutokea makosa ya kiufundi katika tangazo
lililochapishwa leo Alhamisi kwenye gazeti moja la serikali.
Alisema,
tarehe iliyotangazwa ya Agosti 19, siyo ile iliyoamriwa na mahakama,
kwa usahihi jengo hilo lililopo maeneo ya Jangwani jijini Dar es Salaam,
lilitakiwa kupigwa mnada leo Agosti 17.
MCL Digital,
iliwatafuta viongozi wa Yanga, katibu mkuu, Charles Mkwasa na Ofisa
Habari, Dismas Ten, simu ziliita bila mafanikio.
Timu
ya Yanga kwa sasa ipo kambini Pemba ikijindaa na mchezo wake waNgao ya
Jamii dhidi ya Simba utakaofanyika Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment