Saturday 5 August 2017

UMOJA WA MATAIFA WAUNGA MKONO VIKWAZO VIPYA DHIDI YA KOREA KASKAZINI

Kombora la Korea Kaskazini
Baraza la usalama la Umoja wa mataifa, limechukua hatua madhubuti ya kuiadhibu Korea Kaskazini kwa hatua yake ya mwezi uliopita ya kuifanyia majaribio zana zake za kitonoradi.
Katika kura ya pamoja, baraza hilo limeidhinisha vikwazo vipya, vinavyolenga biashara ya chuma na mkaa ya mawe ya Pyongyang--ambayo huuza nje bidhaa hizo kwa zaidi ya dola bilioni kwa mwaka.
Rais wa Marekani Donald Trump, alipongeza hatua za China na Urusi za kuunga mkono vikwazo hivyo vilivyotolewa na baraza hilo la Umoja wa mataifa.
Anasema kuwa, vikwazo hivyo, vitakuwa na "athari kubwa mno" ya kibiashara.
Majirani wao Korea Kusini, wameiomba Korea Kaskazini kufuata njia ya mazungumzo, ili kutanzua mzozo uliopo wa mpango wa Pyongyang, kuhusu zana za kinuklia.
Beijing pia inaomba kurejelewa kwa mazungumzo.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive