Saturday, 5 August 2017

UMESIKIA ALICHOSEMA TUNDU LISSU?


Tundu Lissu amesema kuna double standard imetumika kuwavua ubunge wabunge wa CUF, Amesema ikitokea wabunge wa upinzani wakitumiwa na CCM kuvuruga chama na upinzani ukaamua kuwafukuza spika haridhii kuwafukuza hadi kesi zinafunguliwa mahakamani

Imetokea wabunge wa CUF wamefukuzwa uanachama na Lipumba na kuna mgogoro kati ya usahihi wa uenyekiti wake kisheria na usahihi wa maamuzi ya kikao walichokaa ila Spika anawafukuza haraka haraka akijua kuna mgogoro
Amehoji iwapo mahakama kuu itatoa uamuzi kubatilisha uenyekiti wa Lipumba hao wabunge walioteuliwa na kikao hicho watafukuzwa tena?
Amesema wakiapishwa watakua ni wabunge wa CCM na kambi rasmi ya upinzani haitawatambua kama wabunge wa upinzani

Amesema wanafanya hivyo kwa sababu lengo lao ni kuua upinzani, na Magufuli alishamtamkia spika hadharani kuwa awashughulikie wapinzani ili kufuta upinzani kibaki chama kimoja amambacho ameita hizo ni enzi za giza na haitawezekana

Ameongeza kuwa Lipumba anaweza kufanikiwa kuiteka CUF na kuuwa UKAWA lakini hiyo inaweza kuwaunganisha wapinzani wa kweli
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive