KIUNGO mshambuliaji Ramadhan Singano ambaye alikuwa akiichezea Azam
FC, Alhamisi mchana alirejea nchini akitokea Morocco alikokwenda kwa
ajili ya kucheza soka la kulipwa katika timu ya Difaa Al Jadida.
Akiwa Morocco kwenye mipango yake hiyo inaelezwa kuwa wakala wake
amechangia kukwama kwa dili la kujiunga katika kikosi hicho na ndiyo
maana amerejea Dar ambapo moja kwa moja amekutana na ofa ya kusajiliwa
na Yanga. Singano aliondoka hapa nchini Julai 14, mwaka huu, alikwenda
Morocco kwa makubaliano ya kusaini mkataba wa miaka mitatu katika timu
hiyo, lakini alishangaa kufika huko na kutakiwa kufanya majaribio ambapo
alicheza mechi sita.
Mtu wa karibu wa mchezaji huyo, alisema: “Singano amerejea baada ya
wakala wake anayeitwa Khalid kuwa na tamaa ya fedha kutokana na
kupandisha dau na kwenda kinyume na makubaliano kitendo ambacho ile timu
imekasirika. “Sisi kama watu wake wa karibu, tumemwambia arudi awahi
dirisha la usajili hapa nyumbani kabla halijafungwa na kama ikitokea
anahitajika tena ataondoka,” alisema mtu huyo.
Aidha kaka yake Hamis Singano aliliambia gazeti hili kuwa, Singano
alikuwa tayari amesaini mkataba wa awali na klabu hiyo, kilichobaki ni
kwenda kumalizika kupimwa afya na masuala mengine ili awe mchezaji wao.
Katika mkataba huo, inaonyesha kwamba kila mwezi Singano angekuwa
akilipwa dola 2,000 (zaidi ya Sh 4.4m) kama sehemu ya mshahara kwa muda
wa miaka mitatu, huku fedha ya usajili kwa kila mwaka ikiwa ni dola
56,000 (zaidi ya Sh 124m).
56,000 (zaidi ya Sh 124m).
Kama dili hilo lingefanikiwa, basi Singano angecheza timu moja na
kiungo wa zamani wa Yanga, Simon Msuva ambaye hivi karibuni alijiunga na
timu hiyo kwa mkataba wa miaka mitatu.
Yanga yamfuata Taarifa ambazo gazeti hili imezipata ni kuwa Yanga
imeshamfuata mchezaji huyo kwa ajili ya kumsajili kwa kuwa mkataba wake
na Azam FC ulimalizika mwezi uliopita.
Alipotafutwa Singano mwenyewe kuhusu suala hilo, alisema: “Kweli
nipeshapata ofa kadhaa ikiwemo Yanga, kuhusu nitasaini au la
nitakujulisha, nipe muda kwa kuwa ndiyo kwanza nimefika.” Kigogo mmoja
wa Yanga, alisema: “Ndiyo tuna mpango huo wa kumsajili na ninadhani
tutakamilisha dili hilo kabla ya kufungwa kwa usajili maana tumesikia
Azam na Singida United nao wanamuwania.”
0 comments:
Post a Comment