Kiungo wa mpya wa Yanga, Papy Tshishimbi amewasili kisiwani Pemba
tayari kuungana na kikosi hicho kinachojiandaa na mechi dhidi ya Simba
itakayochezwa Jumatano ijayo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Papy aliwasili Pemba saa 9:27 alasiri kwenye Uwanja wa Ndege wa Pemba na kupokelewa na meneja wa kikosi hicho Hafidh Saleh.
Akizungumza
baada ya kuwasili Papy alisema ilikuwa afike mapema kujiunga na timu
yake hiyo, lakini kikubwa kilichomzuia ni kuchelewa kwa pasi yake mpya
ya kusafiria ambayo ilichelewa kutoka baada ya ile ya awali kuwa katika
hatua za mwisho kumalizika.
Papy alisema pamoja na
kuchelewa hajafanikiwa kuipata pasi hiyo kutokana na kulazimika kuwahi
kujiunga na wenzake kujiandaa na mechi dhidi ya Simba.
Kiungo huyo anayetua Yanga akitokea Mbambane Swallows ya Swaziland alisema anahitaji kujifua kwa siku chache kuweka mwili.
Haikuwa
kazi rahisi kwake kuondoka Mbambane kutokana na klabu hiyo bado
inamuhitaji na kuwalazimu baadhi ya marafiki na mashabiki kulia na
kuwapigia makelele viongozi wa klabu yake, lakini aliamua yeye binafsi
kutaka kubadili maisha kwa kuhamia klabu nyingine.
"Nimefurahi
sana kuwa hapa, nimekuja kuitumikia Yanga naamini nitafanya kazi ambayo
mashabiki wa Yanga wataifurahia nimeambiwa walikuwa
wananisubiri,"alisema Papy.
0 comments:
Post a Comment