Hatma ya wachezaji kiungo wa Singida United Deus Kaseke na
mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa itajulikana alhamis ijayo baada ya
kikao cha kamati ya saa 72.
Kaseke na Chirwa
walismamishwa kucheza baada ya kutuhumiwa kufanya fujo katika mechi ya
mwisho ya Ligi Kuu msimu uliopita katia ya Yanga dhidi ya Mbao FC.
Ofisa Habari wa TFF alisema kikao hicho kitatoa uamuzi juu ya shauri hilo.
"Kikao
kimechelewa kwa sababu ya uchaguzi na kubadilishwa kwa kamati za TFF,
lakini mtakumbuka wachezaji hawa walisimamishwa kwenye mechi ya mwisho
msimu uliopita,"alisema Lucas.
Kutokana na adhabu hiyo
Kaseke alikuwa jukwaani wakati Singida United ikipokea kipigo cha mabao
2-1 kutoka kwa Mwadui, kama ilivyokuwa kwa Mzambia Chirwa aliyeshindwa
kuichezea Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba pamoja na
mechi ligi dhidi ya Lipuli wakitoka sare 1-1.
0 comments:
Post a Comment