Chelsea wanazidi kupata uhakika wa kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kwa pauni milioni 35. (Evening Standard)
Chelsea wamempa masharti kadhaa Diego Costa, 28, ambayo lazima ayatimize ili waweze kumuuza. (Guardian)
Chelsea wanapanga kutumia pauni milioni 120 kusajili wachezaji watatu, Alex Oxlade-Chamberlain, Virgil Van Dijk na Danny Drinkwater. (The Mirror)
Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson amesema atajaribu kumshawishi Philippe Coutinho, 25, asiondoke na kujiunga na Barcelona. (Daily Mirror)
Borussia Dortmund wamekubali dau la euro milioni 100 kutoka kwa Barcelona ili kumsajili Ousmane Dembele, 20, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana kuhusu marupurupu. (SPORT)
Beki wa kati wa Southampton Virgil Van Dijk, 26, ana uwezekano mkubwa wa kuhamia Chelsea au Manchester City kuliko Liverpool, huku Southampton wakitaka zaidi ya pauni milioni 70 kumuuza mchezaji huyo. (Yahoo)
Manchester City wanajiandaa kupanda dau la pauni milioni 60 kumtaka mshambuliaji wa Aresenal Alexis Sanchez, 28. (The Telegraph)
Beki wa Ajax Davinson Sanchez, 21, ameiambia klabu yake kuwa anataka kuhamia Tottenham kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)
Chelsea pia wanamtaka Davinson Sanchez, lakini Ajax wamesisitiza kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia hauzwi. (Daily Star)
Newcastle wanatarajia kumsajili winga wa Chelsea, Kenedy, 21, kwa mkopo, lakini Antonio Conte anasita kumuachia aondoke kwa kuwa kikosi chake kina wachezaji wachache. (Goal)
Juventus wanamtaka kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25. (Gazzetta dello Sport)
0 comments:
Post a Comment