Kiungo mshambuliaji wa PSG Javier Pastore, amempa Neymar namba yake ya jezi - 10- akisema "anataka ajisikie yuko nyumbani". (Tovuti ya PSG)
Meneja wa Real Madrid anaamini kuwa klabu yake lazima imuuze Gareth Bale, 28, ikiwa inataka kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)
Manchester United wanafuatilia kwa makini hali ilivyo Real Madrid na huenda wakapanda dau la pauni milioni 90 kumtaka Gareth Bale, 28. (Daily Star)
Jose Mourinho anaamini anaweza kumsajili Gareth Bale kwa chini ya pauni milioni 90. (Don Balon)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, atawasilisha maombi rasmi ya kutaka kuondoka Stamfrod Bridge. (Independent)
Wakili wa Diego Costa ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Chelsea baada ya klabu hiyo kupinga Costa kwenda AC Milan kwa mkopo kabla ya kwenda Atletico Madrid mwezi januari. (Mirror)
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Edin Hazard, 26, amewasiliana na Barcelona kuhusu kwenda kuziba pengo la Neymar. (Don Balon)
Chelsea wapo tayari kupambana na Liverpool katika kutaka kumsajili beki wa kati wa Southampton Virjil van Dijk, 26, kwa kutoa pauni milioni 50. (The Times)
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, huenda akakosa mechi za mwanzo za msimu kutokana na hatma yake kutofahamika. (Telegraph)
Jurgen Klopp amekuwa na mawasiliano ya karibu na Kylian Mbappe, 18, huku Liverpool wakiendelea kumfuatilia mshambuliaji huyo wa Monaco. (L'Equipe)
Meneja wa Everton Ronald Koeman bado ana matumaini ya kusajili mshambuliaji mwingine, huku bado wakiendelea kumtaka Olivier Giroud, 30, wa Arsenal. (Liverpool Echo)
Mabingwa wa Ufaransa, Monaco, wanajiandaa kutoa dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez, 28. (Sun)
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, alibusu nembo ya Arsenal mbele ya waandishi wa habari wakati wa mazoezi siku ya Alhamisi. (Telegraph)
Dau la Arsenal kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20, limekataliwa. (Mundo Deportivo)
Borussia Dortmund wapo tayari kuzungumzia uhamisho wa Ousmane Dembele, 20, kwenda Barcelona, ikiwa tu Barca watakuwa tayari kutoa euro milioni 100. (Bild)
Kiungo wa Bayern Munich Arturo Vidal anataka kurejea Italy, baada ya kufikia makubaliano na Inter Milan. (FCInterNews)
Meneja wa Crystal Palace Frank de Boer anataka kumsajili beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 19. (Sun)
Anderlecht ya Ubelgiji wameingia katika mbio za kumsajili beki wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen, 31 ambaye pia anasakwa na West Brom. (Birmingham Mail)
0 comments:
Post a Comment