Friday 25 August 2017

MAHUJAJI WA MECCA WATAPELIWA DAR, WAKWAMA AIRPORT

BAADHI ya mahujaji waliokuwa wamejiandaa kwa ajili kwenda Mecca nchini Saudi Arabia, wamekwama katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar kufuatia visa, passport na tiketi zao kutokuwa tayari kwa ajili ya safari hiyo.
Wakizungumza LIVE na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, mahujaji hao wamesema walitakiwa kuondoka hapa nchini kuelekea Mecca na ndege ya saa 8 mchana lakini cha kushangaza imeshindikana kwa kuwa taasisi walioilipa fedha ili kuwakamilishia taratibu zote za safari hiyo viongozi wake wameingia mitini na kuwaachia mabegi matupu.
Mahujaji hao wanaeleza kusikitishwa kwao na kile walichokiita kuwa ni utapeli huku wakifanya kila jitihada za kuwasiliana na viongozi wa taasisi hiyo lakini simu zao hazipokelewi na wengine zinapokelewa na wafanyakazi wao wa ndai huku wakiwaeleza kuwa wahusika wa simu hizo hawapo jambo ambalo wameshindwa cha kufanya, hivyo wameamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive