Kikosi cha Yanga SC.
MLAN-DEGE FC hivi karibuni ilifungwa mabao 2-0 na Yanga, halafu
ikatoka suluhu na Simba, sasa kocha wa timu hiyo Jaala Abdallah Salum
amesema Yanga ipo vizuri kuliko Simba katika fiziki.
Simba na Mlandege zilitoka suluhu usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika
mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Amaan ambapo kabla ya
mechi hiyo Mlandege ilifungwa mabao 2-1 na Yanga ambayo wafungaji wake
walikuwa Ibrahim Ajibu na Emmanuel Martin.
Wachezaji wa timu ya Yanga.
Katika kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Jumatano ijayo
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kocha huyo amesema Simba
itabidi irekebishe baadhi ya mambo kama inataka ushindi.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Salum alisema
timu yake ilitoka sare na Simba kutokana na fiziki yao kuwa juu kuliko
wapinzani wao hali ambayo ni tofauti na walipocheza na Yanga.
“Mechi yetu na Simba ilikuwa nzuri kwetu kwani tuliwazidi katika
fizikia maana wao ilioneka ipo chini tofauti na sisi, lakini Yanga
walitusumbua kwa sababu walikuwa na fiziki kuliko sisi.
“Yanga walikuwa fiti kuliko sisi walikuwa na nguvu na kasi katika
muda wote wa mchezo, Kocha wa Yanga George Lwanda-mina ni mjanja sana
kwa sababu alianza kuwatumia vijana, wakatu-chosha.
“Halafu akawaingiza wale ambao ni wazoefu ikawa shida kwetu ila
kikubwa ilikuwa fizikia yetu ipo chini, nadhani Simba huenda katika siku
hizi mbili wakawa vizuri kabla ya mchezo na Yanga vinginevyo itakuwa
tabu kwao,” alisema Salum.
0 comments:
Post a Comment