Dar es Salaam. Afisa
Habari wa Simba, Haji Manara alisema klabu hiyo haijaafikiana na
mawakala wa mchezaji Shiza Kichuya ili kumpeleka kucheza soka la kulipwa
nchini Misri.
"Wakija na ofa tunayotaka wala hatuna
shida, Simba tuna utamaduni wa kuuza wachezaji,"alisema Haji bila kutaja
kiasi ambacho Simba inahitaji.
MCL Digital
lilizungumza na Kichuya ambapo alisema yeye ni mchezaji na ataufanyia
kazi uamuzi utakaoafikiwa baina ya klabu yake na mawakala na kusisitiza
anafurahia maisha kweny kikosi cha Simba.
Klabu ya
Etihad ya Misri ndiyo inayotajwa kuwania saini ya Kichuya baada ya
kumuona kwenye mashindano ya Cosafa yaliyofanyika nchini Afrika Kusini
mwezi uliopita.
Pia, Manara alisisitiza kuwa beki
Juuko Murshid bado mchezaji wa Simba na atakiwa kuripoti Dar es Salaam
kabla timu haijaenda Zanzibar.
"Bado ana mkataba na
sisi wenzetu walitaka afanye majaribio, lakini sisi tuliona muda
unakwenda na tunamhitaji kikosini,"alifafanua Haji.
SOURCE: MWANASPOT
SOURCE: MWANASPOT
0 comments:
Post a Comment