Thursday, 31 August 2017

HOFU YA MBOWE YAONEKANA KWA WATAKAOWANIA URAISI 2020!!!


Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, amefuta mchakato wa kuwapata viongozi katika kanda za chama hicho, kutokana na zoezi hilo kuingiliwa na kambi zinazojiandaa kumweka mgombea urais kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.


Taarifa iiliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vicent Mashinji, inawataka wanachama wake kufuta maandalizi yote yaliyokwishafanyika mpaka hapo Mh. Mbowe atakapoamua tena.

Taarifa hiyo pia imeongeza kuwa Mh. Mbowe amefuta matokeo ya uchaguzi uliokwishafanyika mwaka huu kutokana na uwepo wa misuguano ya vita ya urais wa mwaka 2020
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive