Zanzibar imefutiwa uanachama wake
katika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ikiwa ni miezi minne tu imepita
tangu walipokubaliwa na kuwa mjumbe wa shirikisho hilo.
Rais wa CAF, Ahmad Ahmad amesema kwa,
Zanzibar ambayo ni sehemu ya Tanzania haikupaswa kabisa kukubaliwa kuwa
mjumbe wa 55, uamuzi uliofanywa Machi 2017.
Rais huyo amesema kuwa, Zanzibar
ilikubalia kuwa mwanachama wa CAF bila kuzingatiwa kwa vigezo vya msingi
ambavyo ni muhimu, huku akifafanua zaidi kuwa, CAF haiwezi kuvikubalia
vyama viwili vya soka kutoka nchi moja.
CAF imesema kuwa kigezo chao cha kutambua nchi ni ile inayotambuliwa na Umoja wa Afrika (AU) pamoja na Umoja wa Mataifa (UN).
Licha ya kuwa Rais wa CAF aliyepita,
Issa Hayatou aliikubalia Zanzibar kuwa mwananchama, lakini Shirikisho la
Soka Duniani (FIFA) lilikataa kuifanya Zanzibar kuwa mwanachama.
Zanzibar ni sehemu ya Tanzania lakini
kwenye masuala ya mpira imekuwa ikijitegemea. Katika mashindano ya
kanda, imekuwa ikishiriki kama nchi.
0 comments:
Post a Comment