Mama Diamond (wa tatu kushoto) akiwa na mkwe wake, Zari (kushoto kwake).
Waombolezaji wakiswali msibani.
Mama mzazi wa Zarina Hassan, Halima Hassan aliyefariki dunia jana asubuhi, baada ya kuugua kwa wiki kadhaa na
kulazwa hospitali amezikwa leo Julai 21, 2017 katika Kitongoji cha
Munyonyo, Kampala.
Kina mama wakiomboleza.
Alhamisi iliyopita
Ushindi Media ililiripoti hali ya ugonjwa ya mama huyo kutokuwa nzuri baada ya kudaiwa kupumulia mashine ya oksijeni kwenye
Kitengo cha Wagonjwa Mahututi (ICU) katika Hospitali ya Nakasero iliyopo nchini
Uganda akisumbuliwa na maradhi ya
moyo na figo ambayo yamekuwa yakimsumbua tangu kufariki kwa mkwe wake, Ivan Ssemwanga.
Hali ilivyokuwa nyumbani kwa mama Zari.
Kwa mujibu wa chanzo ndani ya familia hiyo, mama
Zari alipata matatizo ya
moyo na figo baada ya kuanguka ghafla na kichwa chake kujigonga, hali iliyosababisha akimbizwe hospitalini haraka.
Kaburi ambamo mwili wa marehemu utazikwa.
Kifo cha mama
Zari ambaye alizaliwa
Mei 15, 1959, kimekuja ikiwa ni takribani miezi miwili tu tangu mkwe wake,
Ivan Semwanga, aliyeaga dunia
Mei 25 mwaka huu huko
Steve Biko Academic Hospital nchini
Pretoria, Afrika Kusini.
Waombolezaji wakijumuika na Zari na mama Diamond.
Waombolezaji wamefurika nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kushiriki
mazishi ya mama huyo ambaye amekuwa maarufu Afrika Mashariki na Kati
kupitia kwa mwanaye Zari.
Chakula kikipakuliwa.
Dada wa Zari, Zuleha Hassan akiomboleza kifo cha mama yake.
Jeneza lenye mwili wa marehemu likishushwa kwenye gari.
Jeneza likipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa na kufanya taratibu za mazishi.
Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu.
Swala kwa ajili ya marehemu.
Kundi la matajiri lijulikanalo kama Rich Gang wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu.
Mmoja wa waombolezaji akigonga pilau.
Pumzika kwa Amani, Halima Hassan.
0 comments:
Post a Comment