WAKATI mbiombio za usajili zikiendelea, habari ni kuwa klabu ya Yanga imeamua kuachana na mpango wa kumsajili beki wa Mbao FC, Yusuph Ndikumana na sasa imeelezekeza nguvu kumuwania beki kutoka Nigeria.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na kushindwana na Ndikumana katika masuala ya kimaslahi, hivyo uamuzi wa kumuwania Mnigeria huyo umekuja kama mbadala.
“Ni kweli kuna beki raia wa Nigeria,
yupo vizuri hasa, tumekuwa tukimfuatilia kwa miezi kadhaa, mazungumzo
yameanza na kuna uwezekano akaja siku yoyote kuanzia kesho (leo
Ijumaa),” alisema mtoa taarifa kutoka ndani ya Yanga.
Ikumbukwe kuwa Yanga imekuwa ikihitaji beki wa kati kutokana na kuachana na Vincent Bossou aliyekuwa nguzo muhimu katika nafasi hiyo, huku umri ukionekana kumtupa mkono nahodha,Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Aidha, wakati tukiingia mitamboni kulikuwa na taarifa kuwa Yanga ipo katika mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Azam FC, Kipre Tchetche ambapo inadaiwa tayari mazungumzo yameshaanza kufanya na kuna uwezekano wa kuwafanyia mashabiki wao ‘sapraizi’ ya kumsajili.
0 comments:
Post a Comment