Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe leo Julai 10 amesitisha uteuzi wa mwenyekiti pamoja na wajumbe wote wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuanzia leo kwa mamlaka aliyopewa na sheria ya BMT Na.12 ya 1967.
Mwakyembe ameeleza kuwa sababu ya
kusitisha uteuzi huo inatokana na agizo alilopewa na Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa aliyemwagiza afanyie kazi mapitio na kulitathmini upya baraza
hilo ili kujiridhisha na usimamizi wake kuhusu michezo.
Kutokana na kujiridhisha kwake kwamba usimamizi wa BMT
si imara, basi ameweza kulivunja na ataliunda upya na kwa sasa
sekretarieti ya balaza hilo itaendelea kufanya kazi katika kipindi hiki
ikishirikiana na wizara.
0 comments:
Post a Comment