KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amefunguka kwa sasa anaendelea na mazoezi na kikosi hicho ambapo
mashabiki ambao wana hofu na uwezo wake wamsubiri uwanjani kwenye mechi
dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda, kwenye mechi ya Simba Day.
Mganda huyo amefanikiwa kurejea kwa mara nyingine ndani ya Simba kwa
mkataba wa miaka miwili akitokea Villa ya Uganda ambapo kwa sasa yupo
nchini Afrika Kusini kwenye kambi ya timu hiyo chini ya kocha wake,
Joseph Omog raia wa Cameroon.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Okwi
mmoja wa wachezaji waliokuwepo kwenye ubingwa wa mwisho wa Simba,
amesema anaendelea na mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo wa Simba Day dhidi ya Rayon ambao ndiyo utakuwa wa kwanza ndani
ya kikosi hicho tangu kurejea kwake.
“Tunaendelea na mazoezi ya pamoja ya
kujiandaa na msimu ujao, lakini kwa wale ambao wana hofu juu ya nini
nitakachokifanya basi niwaambie kuwa nitawaonyesha makali yangu kwenye
mechi ya Simba Day ambayo itakuwa ya kwanza kwetu nchini Tanzania,”
alisema Okwi aliyewahi kucheza soka la kulipwa Denmark.
0 comments:
Post a Comment