Watu wawili wenye umri wa miaka 30 akiwemo baba aliyetaka kumuuza mwanawe ili kupata fedha za kuandaa mazishi ya marehemu mamake walishtakiwa katika mahakama ya Iyaganku mjini Ibadan Nigeria.
Kulingana na gazeti la Vanguard nchini humo washtakiwa hao walishtakiwa na mashitaka mawili ya kupanga njama na jaribio la kuuza mwanawe wa kiume wa miaka sita
.Wakati mashtaka hayo yaliposomwa wote walikana kufanya hivyo.
Kulingana na gazeti hilo kisa hicho cha kushangaza kilitokea katika eneo la Agbowo mnamo mwezi Juni tarehe 21.
Kulingana na kiongozi wa mashtaka, sajenti Oriola James, babake mvulana huyo na rafikiye walipanga njama za kumuuza mtoto huyo.
Gazeti la Vanguard linasema kuwa mmoja ya washukiwa hao alidaiwa kuwaambia maafisa wa polisi kwamba mamake alifariki na kwamba alikuwa anatafuta fedha za kuandaa mazishi yake.
Huku asijue kitu cha kufanya alimwita rafikiye kutafuta mtu ambaye anaweza kumnunua mwanawe ili kuchangisha fedha za mazishi hayo.
Alielezea kwamba rafikiye alimwambia kwamba amepata mnunuzi wa mvulana huyo.
Lakini mtu aliyetakiwa kumnunua aliwaelezea maafisa wa polisi kuhusu njama hiyo .
Wawili hao waliachiliwa kwa dhamana Naira 100,000 hukju mahakama ikipanga kesi hiyo kusikizwa Agosti 31.
0 comments:
Post a Comment