Mbunge wa Sengerema kwa tiketi ya CCM, William Ngeleja amerudisha
pesa kiasi cha Tsh milioni 40.4 alizohusishwa nazo kwenye sakata la
Tegeta Escrow.
Pesa hizo inadaiwa kuwa alipewa mgao yeye na baadhi ya wabunge pamoja
na viongozi wengine wa serikali, dini na majaji kutoka kwa James
Rugemalira wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd.
Taarifa ya kurudisha fedha hizo ameitoa leo mbele ya waandishi wa
habari ambapo alisema lengo la kuzirudisha ni kuhusishwa kwake na kashfa
kuchotwa kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.
Ngeleja amedai kuwa fedha hizo alipewa msaada kama ilivyokuwa wabunge
wengine waliogawiwa na James Rugemalira kwa ajili ya maendeleo ya jimbo
lake la Sengerema.
This comment has been removed by the author.
ReplyDelete