Baada ya tambo nyingi zilizoletwa na ushindi wa michezo yao
yote ya kujiandaa na msimu wa ligi hatimaye usiku wa kuamkia leo ngebe
za mashabiki wa Manchester United zilitulizwa.
Manchester United walikuwa uwanjani katika mchezo wao wa mwisho
barani America waliocheza dhidi ya wababe wa kutoka Hispania klabu ya
Barcelona.
Mchezo ambao ulijaza mashabiki wengi na huku watu wengi waliutazama
kutokana na fomu ya sasa ya United na ubora ambao wakonao klabu ya
Barcelona.
Alikuwa
Neymar Dos Santos mchezaji anayezungumzwa sana kwa sasa na vyombo vya
habari ndiye aliyeimaliza United katika dakika ya 31 ya mchezo.
United kupitia kwa Lukaku na Rashford walijitahidi sana kulishambulia
sana lango la Barcelona lakini umahiri wa golikipa Jasper Cillessen
ulizizima jitihada za United.
United sasa wanarudi barani Ulaya kwa michezo miwili ya kirafiki zidi
ya Vilarenga nchini Norway na ule zidi Sampdoria kabla ya kukutana na
Real Madrid katika fainali ya Super Cup.
Katika
mchezo mwingine mkubwa wa kirafiki PSG walikubali kipigo cha mabao 3
kwa 2 toka kwa Juve huku Claudio Marchisso akiifungia Juve mara
mbili,Higuain moja na yale ya PSG yakifungwa na Goncalo Guede na Javier
Pastore.
0 comments:
Post a Comment