Thursday, 27 July 2017

MANARA AIPAISHA SIMBA


Uongozi wa Klabu ya Simba wenye makao makuu yake Msimbazi Jijini Dar es Salaam umekanusha vikali taarifa iliyotembea katika mitandao ya kijamii inayodai timu hiyo imechapwa bao 7-0 katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Royal Eagles ya nchini Afrika Kusini walipoweka kambi yao.

Hayo yameweka bayana na taarifa iliyotolewa na msemaji wa timu hiyo Haji Manara na kusema kama kweli wamechezea kichapo hicho kutoka kwa timu ya daraja la kwanza hakuna mtanzania asingeweza kuona matokeo hayo katika vyombo vya habari kutokana na sasa utandawazi umetawala.

"Kiukweli Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani na haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo, kama zilivyo timu nyingine nchini hususan Klabu ambayo mashabiki wake ndiyo wanaozusha upuuzi huo", amesema Manara.

Kwa upande mwingine, Manara amewataka watanzania na mashabiki wa wekundu wa msimbazi watambue kuwa siku zote walizokuwa huko nchini Afrika Kusini, benchi lake la ufundi limejikita katika kutengeneza miili ya wachezaji kistamina ili iweze kufanya vizuri katika michezo yake ambayo ipo usoni kuanza.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive