Salma Mwasa .
Mbunge wa Viti Maalumu (CUF) aliyevuliwa ubunge hivi karibuni Salma Mwasa amesikitishwa na kitendo cha askari wa Manispaa ya Ubungo cha kutaka kumzuia asikanyage kwenye halmashauri hiyo.
Mwasa ni miongoni mwa wabunge kumi waliovuliwa uanachama sanjari na madiwani wawili wa CUF kwa madai ya kukihujumu chama hicho, hali iliyosababisha kukosa fursa za kuwa wabunge.
Akisimulia tukio hilo lililotokea leo Jumatatu, Julai 31, Mwasa
amesema aliitwa na askari hao na kuambiwa hatakiwi kuonekana katika
eneo hilo la manispaa na kwamba, hiyo ni amri kutoka juu kwa wakubwa.
“Mimi ninachojua amri zipo kumi tu,
sasa hiyo 11 inatoka wapi? Lakini niliwaeleza kwamba mimi ni mkazi wa
Ubungo sasa mnaponizuia nisije hapa hamnitendei haki kwa sababu nakuja
kufanya mahitaji mbalimbali,” amesema.
“Mimi nimekuja kama mwananchi wa
kawaida. Naomba umma utambue mimi bado ni mbunge hapa nilipo nina barua
ya uteuzi na sina barua ya utenguzi,” anasema Mwasa.
Hata hivyo, haikuwa rahisi askari hao
wa manispaa kumtambua Mwasa badala yake walikuwa na karatasi yenye
majina mawili yaliyoandikiwa Salma Mwasa na diwani wa viti maalumu Leila
Hussein, ambao hakutakiwa kuonekana eneo hilo wakati kikao cha Baraza
Madiwani kikiendelea.
Askari hao walitumia njia za kuwauliza
watu mbalimbali wakiwamo waandishi kama wanawafahamu kina Mwasa na Leila
na walipowauliza wanashida nao gani walijibu hawatakiwi kuingia ndani
ya ukumbi wa mikutano.
0 comments:
Post a Comment