Mshambuliaji
mpya wa Yanga, Ibrahim Ajibu amezua mjadala kwenye mtandao wa kijamii
baada ya kutuma ujumbe akimshukuru Mungu na kusema anajiamini.
Baada
ya hapo mashabiki wameanza kutuma maoni yao kila mmoja akisema yake
lakini walioonekana ni wa Simba, walikuwa wakimshangaa au kumlaumu
kuhama huku wengine wakimuita ni msaliti.
Waliomuita msaliti walisema amehama lakini hataweza kucheza soka katika kiwango bora.
Lakini wale walioonekana ni wa Yanga walimpa moyo na kumtaka acheze bila ya woga kwa kujituma huku wakimkaribisha.
Baadhi
yao walifikia kushangazwa na wale waliiwaowahi kumuita anajua sana
akiwa Simba lakini kwa kuwa amehama anaonekana hana lolote.
Wakati
mwingine, mashabiki hao walianza kubishana au kuzoana wao kwa wao
wengine wakionyesha kuwa na jazba wakati wakiwajibu wengine.
Pamoja na rundo la maoni, Ajibu aliendelea kuwa kimya bila kusema lolote.
0 comments:
Post a Comment