Thursday 20 July 2017

KAULI YA WAKILI KIBATALA BAADA YA LISSU KUKAMATWA


Leo July 20 Mwanasheria, Mbunge wa CHADEMA na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika TLS, Tundu Lissu amekamatwa akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Rwanda kwenye mkutano wa Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki.

Ushindi Media imempata Wakili wake Peter Kibatala na amezungumzia tukio hilo ambapo amesema kuwa ”Mimi sijaongea naye moja kwa moja kwa sababu simu zake ni ama zimezimika au zimezimwa lakini taarifa nilizopata kutoka kwa watu wake wakiwemo ambao wamemuacha Airport muda si mrefu na wengine ninaowaamini ni yes amekamatwa na anapelekwa Central Police Station.
“Kuna Wakili mwenzangu anaelekea huko kwenda kushughulikia Haki zake za kisheria na pengine kusisitiza kwamba apelekwe Mahakamani na sisi kama ni kweli amekamatwa rai yetu ni hiyo kama wamemkamata na waliomkamata wanaamini kwamba wana tuhuma dhidi yake wakamilishe taratibu zao mapema kama inavyowezekana wampeleke Mahakamani tukakutane naye huko.” – Peter Kibatala.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive