Monday 24 July 2017

FAHAMU HILI KUELEKEA PAMBANO KATI YA MAYWEATHER NA MCGREGOR


Floyd Mayweather vs. Conor McGregor ni pambano ambalo litafafanua vizuri maana ya tukio tajiri la kimichezo mnamo August 26 wakati pambano hili litakapovunja rekodi zote za kifedha zilizowahi kuwekwa huko nyuma katika mchezo huu wa ndondi.

Mnamo mwaka 2015, pambano la Mayweather vs. Pacquiao lilizalisha kiasi cha zaidi ya $600m – sasa tegemea pambano la Mayweather vs. McGregor kutengeneza namba kubwa zaidi ya hizo wakati litakapoonyeshwa kupitia malipo ya kuangalia kwenye TV.

Jarida la Forbes linaripoti kwamba pambano hili litaingiza karibia $1billion – wanasema japokuwa hawajapata namba kamili ila hili ndio litavunja rekodi zote za huko nyuma.

Zaidi ya mashabiki 48,000 walikusanyika katika kumbi za Staples Center, Budweiser Stage, Barclays Center na Wembley Arena kuangalia mikutano ya waandishi wa habari iliyowahusishwa miamba hiyo ya ngumi.

Zaidi ya watu millioni 33 waliangalia mikutano hii kupitia mtandao wa Youtube ulimwenguni kote. Hii yote inakupa picha mvuto mkubwa uliolizunguka hili pambano.

Udhamini wa Pambano la Mayweather-McGregor ni ghali zaidi
Kampuni yoyote inayotaka kuwa mdhamini wa pambano hili inabidi ajiandae kulipa kiasi kikubwa kwa cash. Kwa mujibu wa taarifa za kifedha, kiasi cha kuanzia kujitangaza katika pambano hilo ni $10 million zaidi ya billioni 20 za kitanzania.
Kampuni ya vinywaji ya Tecate walilipa kiasi cha $5.6 million kuwa mmoja wa wadhamini wakubwa wa pambano la Mayweather vs Pacquiao. Kampuni ambayo inakuwa mmoja wa wadhamini wa juu inapata nafasi ya logo yake kukaa katikati ya ulingo katika uwanja wa T-Mobile Arena. Pia kampuni inapata nafasi ya kuwavalisha mavazi yenye logo zao wasichana wa ulingoni, kamba 2 za ulingo na kona ambazo mabondia hawakai. (Neutral corners)
Dili hilo pia litahusisha kuonekana kwa logo kwenye screen kubwa dakika ya kwanza ya kila raundi kwa watu wanaongalia kwenye TV. Rovel pia wanaripoti kwamba kampuni ambayo itataka kudhamini kona za mabondia kwenye ulingo, inabidi walipe kiasi cha $5m.
Ikiwa watauza sehemu zote za udhamini, wataingiza kiasi cha dola millioni 20, ambayo ni dola millioni 7 zaidi ya kiasi kilichopatikana katika pambano la Mayweather-Pacquiao.
Bei za sehemu hizi za kutangazia matangazo ya wadhamini zimetokana na data zilizokusanywa timu ya wajuzi wa masuala ya masoko ya kawaida na upande wa mitandao ya kijamii.
Inaripotiwa kwamba endapo pambano hili litapata mafanikio ya kiuchumi kiasi kile au kupitiliza mafanikio ya pambano la Mayweather vs Pacquiao, basi mapato ya jumla ya bondia Floyd Mayweather yatafikia billioni 1 za kimarekani tangu alipoanza mchezo huu wa ndondi. Hivyo atakuwa mwanamichezo wa 3 baada ya Michael Jordan (1.5 billion) na Tiger Woods (1.4 b) kuwahi kuingiza mapato zaidi ya billion moja ya Trump.
Malipo ya kuangalia kwenye TV ya pambano la Mayweather-McGregor
Jumla ya mapato yaliyopatikana kwa watazamani waliolipia kuangalia pambano la Mayweather-Pacquiao yalikuwa makubwa sana kwa vituo vya HBO na ShowTime. Inakadiriwa jumla ya nyumba millioni 6 nchini Marekani na Uingereza zililipia kuangalia pambano hilo. Malipo kwa nyumba yalikuwa $100 kwa kupata matangazo ya HD na $90 kwa matangazo ya kawaida, kwahiyo ilikusanywa jumla ya $430 million, karibia trillioni 2 za kitanzania.
Sasa pambano la Mayweather-McGregor inaaminika yatapatikana mapato makubwa zaidi, na safari kituo cha ShowTime kitakuwa hakina ushirikiano na kituo kingine cha kimarekani.
Mpaka sasa haijafahamika malipo ya safari hii kwa kila nyumba itakuwa kiasi gani lakini inakadiriwa itakuwa imeongeza kwa kiasi cha $5 mpaka $10.
Uwanja mkubwa zaidi utatumika kufanyikia pambano la Mayweather-McGregor.
Hapa tunaangalia mauzo ya tiketi. Tiketi kwa pambano la Mayweather vs. Pacquiao zilikuwa zinaanzia $1,500 mpaka $10,000. Matokeo yake mzigo uliongia kupitia mauzo hayo ilikuwa ni $73million. Tiketi za pambano hili zilianza kuuzwa siku 9 kabla ya pambano kufanyika – pambano hili lilifanyika katika ukumbi wa MGM Grand ambao unaingiza watu Zaidi ya watu 17,000..
Pambano la Mayweather-McGregor litafanyika katika ukumbi wa T-Mobile Arena ambao unachukua watu 20,000. Siti zaidi ya 3000. Ikitokea viingilio vikawa vile vile kama pambano la mwaka juzi la MayPac basi kwa kiingilio cha chini pekee itaongezeka $4.5 million.
Wakosoaji wa pambano Mayweather Vs. McGregor wanasaidia sana
Wakosoaji wanasaidia sana kulipromoti hili pambano. Watu kama Oscar De La Hoya na hata Pacquiao wanalikosoa sana hili pambano wakisema sio sahihi kwa wapiganaji hawa wawili kupambana. Yoyote ambaye anajua masuala ya mapambano ya kombati anaweza kukubaliana nao, lakini wanapolizungumzka pambano hili ndivyo wanavyozidi kulipa ukubwa. Pia wapo watu wengine wanaoamini McGregor ana uwezo kuhamisha uwezo kwenye ndondi na kumdunda Mayweather katika mchezo – wanazidisha majadiliano ambayo yanakuza ufahamu wa watu kuhusu pambano hili.
Umaarufu wa McGregor duniani ni jambo chanya sana
Pamoja na ukubwa alionao Pacquiao, lakini hana ufuasi mkubwa wa mashabiki katika nchi kubwa kama Uingereza kwa ujumla kama ilivyo kwa McGregor ambaye ni raia wa Uingereza.
Inaripotiwa kwamba McGregor ana ufuasi wenye nguvu na mahaba ya dhati kwake kuliko mashabiki wa mchezo wowote nchini Uingereza. Umaarufu wake huu unaenda nje ya mipaka ya Malkia – kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa michezo ya UFC utakubaliana nami kuhusu mashabiki wa McGregor na kwa maana pambano lake na MayWeather litaongezeka zaidi.
Malipo kwa Mabondia – Mayweather – McGregor
Jarida la Forbes linaripoti ikiwa kutakuwa na mafanikio makubwa katika watazamaji watakaolipa kuangalia pambano hili kwenye TV, basi huenda pambano hili likaingiza karibia billioni 1 za kimarekani.
Makubaliano ya pambano hili kwenye malipo inakadiriwa kuwa na mgawanyo wa 70-30, Mayweather akichukua mpunga mrefu zaidi ya McGregor.
Endapo mambo yataenda kama inavyotarajiwa basi huenda Mayweather akapata zaidi ya dola millioni 250 (kiwango cha juu zaidi $400) alizopata wakati wa pambano la MayPac, huku mpinzani wake McGregor akiondoka na $75m kwa kiasi cha chini na juu zaidi $175m.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive