Monday, 10 July 2017

CHADEMA WATOA TAMKO JUU YA NGELEJA...


Leo TAIFA limeshuhudia kituko kingine cha Karne baada ya Mbunge WA Sengerema William Mganga NGELEJA kuitisha waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Habari maelezo ambao unamilikiwa na Serikali na kuamua 'Kutakatisha'Fedha haramu za Escrow.


Nasema ametakatisha Fedha haramu Kwani sote tumeshuhudia Ndugu Rugemalila ambaye alimpa NGELEJA hizo Fedha Akiwa kizimbani na moja ya mashtaka aliyopewa ni pamoja na LA 'Kutakatisha ' Fedha .

Njia mojawapo aliyoitumia 'Kutakatisha "hizo Fedha ni pamoja na kuwagawia watu mbalimbali akiwemo William NGELEJA ambaye naye amezirejesha Serikalini badala ya kuzirejesha kwa Rugemalila.

NGELEJA huyu Ametoa sababu ya kurejesha Fedha hizo ni ili kuepuka kashfa na anasema hajawahi kukumbwa na kashfa yoyote . Anasahau kuwa ni juzi tu hapa ripoti ya Prof.Osoro maarufu kama 'Makenikia' ilimtaja Tena kwa Jina kuwa anahusika na ufisadi uliofanyika Katika sekta ya Madini Nchini alipokuwa waziri wa Nishati na Madini. 

NGELEJA huyu alipokea Fedha hizo Mwaka 2014 na Mwaka 2015 baada ya Kelele kuwa Kubwa alilipa Kodi TRA kiasi cha shilling 13 Milioni, kutokana na kipato hicho. 

Leo anajitokeza na kurejesha hizo Fedha serikalini ambako baada ya kuzilipia Kodi maana yake zilikuwa Mapato halali kwake na zilishatakata rasmi! 

NGELEJA ameacha Maswali yafuatayo kwa kitendo chake hiki; 

1. Je ? Kwanini amezirejesha serikalini badala ya kuzirejesha kwa Rugemalila ( ambaye Ana kesi ya Kutakatisha Fedha zikiwamo na hizo alizokuwa amempa NGELEJA?)

2. Je ? Kitendo hiki sio cha kujaribu Kutakatisha hizo Fedha kwa kuzirejesha serikalini na hivyo kuharibu mwenendo WA Kesi?

3.Kwanini Serikali imempa ukumbi wake ili akatolee hapo Tamko LA kurejesha Fedha ambazo Zina kesi ya Utakatishaji fedha Mahakamani? 

4. Hivi kitendo cha Serikali kupokea fedha hizo hakuwezi kuathiri mwenendo wa kesi iliyoko Mahakamani? Kwani naamini kuwa wanufaika wa fedha haramu hizo ni sehemu muhimu ya kesi hii (kesi ya Escrow) 

5.Tunaitaka Serikali iweke wazi fedha hizo zitaingizwa kwenye fungu lipi? Na Je kama Rugemalila ameshitakiwa kwa Kutakatisha fedha ,Hivi Hati ya mashtaka itaenda kurekebishwa na hasa kwenye kiwango cha fedha kwani serikali imeshachukua sehemu ya fedha hizo kama Mapato yake halali ?

6. Kitendo cha Ngeleja kurejesha fedha sio ushahidi tosha wa kumtia hatiani Ngeleja ? Anasalimika vipi huyu na Kesi iliyoko Mahakamani? 

Mwisho ni kwanini Ngeleja amerejesha Milioni 40.4 wakati alishalipia kodi ya Zaidi ya Milioni 13 kutoka kwenye fedha hizohizo? Nyongeza aliyoitoa serikalini ni kwa ajili ya kazi gani? Au ndio kukosa umakini? 

Tunaamini kuwa serikali na Ngeleja watatoa majibu kwa umma juu ya igizo Hili la Ngeleja ambalo linaweza kabisa kuathiri mwenendo wa kesi iliyopo Mahakamani.

Imetolewa Leo tarehe 10 Julai ,2017.

John Mrema 

Mkurugenzi wa Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive