CHAMA cha Mapinduzi CCM wilaya ya Korogwe Mjini, kimetishia kuwatimua wanachama watakaokwenda kinyume na taratibu za chama hicho bila kujali nafasi waliyonayo, umaarufu wala uzoefu wa siku nyingi.
Akizungumza katika mkutano maalumu wa baraza la wazazi wa kujadili majina ya wagombea nafasi mbalimbali, Katibu wa CCM Korogwe Mjini, Ally Issa alisisitiza suala la uadilifu na kwamba hakuna mtu atakayebebwa kutokana na umaarufu wake, cheo wala uzoefu wa siku nyingi ndani ya chama ama Jumuiya zake.
Issa alisema mchakato wa kuwapata watu wa kusimamia kura lazima ufanyike kwa umakini huku akiwataka wasimamizi hao kutenda haki.
Aidha katibu huyo alisema ndani ya chama hicho suala la rushwa halina nafasi na yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo atashughulikiwa kisheria.
0 comments:
Post a Comment