Friday 23 June 2017

TFF KUMUWEKA MTU KATI NYOSSO




SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) kupitia kamati yake ya nidhamu chini ya mwenyekiti wake, Tarimba Abbas, linatarajia kumjadili beki Juma Nyosso aliyetua Kagera Sugar kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo katika msimu ujao.

Beki huyo alifungiwa na TFF akiwa na kikosi cha Mbeya City msimu wa 2015/16 kutokana na kosa la kumdhalilisha mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco wakati wa mchezo baina ya timu hizo mbili.

Kufuatia kukamilisha adhabu yake ya kufungiwa miaka miwili, Nyosso amefanikiwa kusaini mkataba wa kuitumikia Kagera Sugar kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu, hivyo kusababisha TFF kumjadili. Taarifa ambazo gazeti hili limezipata kutoka TFF ni kuwa kamati ya nidhamu inatarajia kukutana wakati wowote kuanzia sasa kwa ajili ya kujadili suala la beki huyo kwa kuwa adhabu yake inafikia tamati Septemba 20.

“Adhabu ya Nyosso inatarajiwa kufikia tamati Septemba 20, mwaka huu, hivyo iwapo kamati hiyo itaafi kiana itamsamehe ili kuweza kumwacha huru aitumikie timu yake mpya,” kilisema chanzo hicho.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive