
Wanasaikolojia wa Chuo Kikuu cha Colorado,
Marekani wamesema kuwa kumshika mkono mtu unayempenda wakati anahisi
maumivu kunasaidia kupunguza hali ya maumivu kwa zaidi ya 60%, kwa
mujibu wa utafiti wao.
Utafiti umeonesha kuwa wanawake wengi waliofanyiwa upasuaji au wakati
wa kujifungua hupunguza mawimbi ya maumivu yatokayo kwenye ubongo
kwenda kwenye mwili iwapo walishikwa mikono na waume zao.
Dr Pavel Goldstein, akielezea hali hiyo inavyoweza kutokea kisayansi amesema cingulate cortex ambayo ni sehemu ya ubongo huchelewa kutuma taarifa kwenye ubongo kuhusu kuwepo kwa maumivu kutokana na uwepo wa homoni ya Oxytocin inayozalishwa iwapo mtu atashikana mikono na mtu wanayependana.
Utafiti pia umeonesha moyo hupungua mapigo na kuwa ya kawaida wakati
wa maumivu makali kutokana na saikolojia ya binadamu kujisikia amani
anapokuwa na mtu anayempenda wakati wa kuumwa. Hivyo, imeonekana ni
muhimu kwa wanaume kuwashika mikono wake zao wakati wa kujifungua.

0 comments:
Post a Comment