Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva.
KIUNGO
mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva amefunguka kuwa, kitendo cha Haruna
Niyonzima kuondoka kikosini hapo, kimemuachia maswali mengi yasiyokuwa
na majibu, hivyo ataendelea kummisi kila kukicha.
Niyonzima ambaye msimu ujao ataitumikia
Simba, ameondoka Yanga baada ya kumaliza mkataba huku akishindwa
kuongeza kutokana na kushindwana kimaslahi na viongozi wake hao wa
zamani.
Haruna Niyonzima.
Akizungumza na moja kati ya vya habari hapa nchini ,Msuva
alisema, kati ya wachezaji wote wa kigeni aliowahi kucheza nao ndani ya
Yanga, Niyonzima ndiye aliyetokea kuendana naye kwa kila kitu.
“Kwa kweli Haruna nilimzoea kupitiliza,
alikuwa kama mtani wangu, hivyo basi kwa hali hiyo iliyotokea, kwa
upande wangu nimeumia sana lakini sina jinsi.
“Kuondoka kwake haimaanishi kwamba
nitashuka kiuwezo, bali nitaendelea kupambana na nitashirikiana na
wengine kama nilivyokuwa nashirikiana naye.“Nitamisi vitu vingi kutoka
kwake, najua hata yeye huko alipo nadhani anafahamu ameniacha kwenye
hali gani, nasema hivyo kwa sababu kati ya wachezaji wa nje niliowahi
kucheza nao, yeye pekee ndiye nimevutiwa naye,” alisema Msuva.
0 comments:
Post a Comment