Kampuni ya Multichoice Tanzania imetoa zawadi ya sikukuu ya Idi kwa kituo chakulelea watoto yatima cha Al-Madinnah kilichopo Tandale jijini Dar es Salaam.Msaada huo wa vyakula na vifaa mbalimbali umekabidhiwa kwa kituo hicho naMeneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo katika hafla fupiiliyofanyika kituoni hapo ambayo pia ilihudhuriwa na mabalozi kadhaa wa DStvakiwemo malkia wa Taarab Khadija Kopa na muigizaji maarufu wa filamu na Tamhtilia ya HUBA , Riyama Alli.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Shelukindo amesema kwa takribanmiaka
mitano mfululizo Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho kwa
mambombalimbali.
Amesema
wanafanya hivyo kwa kutambua kuwa malezi ya watotowaishio katika
mazingira magumu ni jukumu la kila mtu na kila taasisi. “Tunatambuakuwa
jukumu la kuwalea watoto kama hawa ambao kwa sababu moja ama
nyinginewamejikuta katika mazingira magumu ni letu sote. Hawa ni ndugu
zetu, watoto wetu,na pia ni tegemeo kubwa kwa taifa letu, hivyo
kuwasaidia ni jukumu letu”
Amesema
mbali na kwamba Multichoice imekuwa ikikisaidia kituo hicho mara
kwamara kwa kuwapa vyakula na mahitaji mengine, lakini pia waliamua
kufadhiliuanzishwaji wa mradi wa ushonaji ambao unakisaidia kituo hicho
katika kujiingiziakipato. “Tunajua kuwa chakula, malazi na mambo
mengineyo ni muhimu kwa maishaya kila siku ya vijana wetu, lakini pia
tuliona ni busara kuwawekea kamradi japokadogo ambako wataweza kujipatia
kipato. Tumefurahi sana kuona mradi huuunaendelea na tunaamini kuwa
wataweza kuuendeleza na kuukuza ili uwasaidiaZaidi.” Alisema Shelukindo.
Kwa
upande wake Mkuu wa kituo hicho Mama Kuruthum Juma
ameishukuruMultichoice Tanzania kwa msaada wao wa mara kwa mara kwa
miaka mingi sasa.
Amesema
kitendo cha Multichoice Tanzania kukisaidia kitua hicho kwa
mambombalimbali hususan mradi wa ushonaji kumewasaidia sana katika
kujipatia kipatajapo kusaidia gharama za uendeshaji kituo hicho ambazo
ni kubwa.
“Kwa
kweligharama za uendeshaji kituo ni kubwa sana na kama mnavyofahamu
watotowanaolelewa hapa hawana uwezo na wengi wao hawana wazazi, hivyo ni
jukumuletu kuwalea, kuwapa matibabu, na pia kuwasomesha, hili kwa kweli
ni jukumukubwa na tunahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali”
alisema Mama Kuruthum
Amesema
idadi ya watoto imekuwa ikiongezeka lakini kituo hakina uwezo
mkubwakutokana na ufinyu wa eneo na bajeti hivyo akawaomba wadau wengine
kuangaliauwezekano wa kukisaidia kituo hicho ili kiweze kuhudumia
watoto wengi Zaidi.
Naye
Malkia wa Taarabu – Khadija Kopa amesema amefarijika sana
kuonaMultichoice Tanzania inawajali watoto hususan wale waishio katika
mazingiramagumu ambao aghalabu husahaulika na jamii. “Kwakweli
Multichoice Tanzania wamefanya jambo la maana sana. Ni vyema
tukaunganisha nguvu zetu kuwaleahawa watoto wetu kwani nao wana haki
kama watoto wengine” alisema Kopa.
Naye
muigizaji Riyama Ali amepongeza jitihada zinazofanywa na
MultichoiceTanzania pamoja na uongozi wa kituo cha Almadinna katika
kuwasaidia watoto hao.
“Watoto
hawa ni hazina ya taifa. Tukiwasaidia hawa wakakua vizuri, wakapata
elimunzuri, kesho na keshokutwa tutapata wabunge humu, mawaziri,
wakurugenzi,wanamichezo, wasanii na kadhalika. Tushirikiane kuwalea na
hili ni jukumu letu sotena ni kitu kinacholeta Baraka” alisema Riyama.
Kituo
cha Al-Madinnah Orphanage Centre kilianzishwa mwaka 2004 na kwa hivi
sasakituo hicho kinahudumia jumla ya watoto 65 ambapo 40 kati yao ni
wavulana na 25wasichana na wengi wao ni wanafunzi wa shule za msingi.
0 comments:
Post a Comment