Sunday 25 June 2017

MOURINHO APATA MSIBA MZITO




Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anayeandamwa na kesi ya ukwepaji kulipa kodi amejikuta katika balaa jingine kubwa zaidi baada ya kumpoteza baba yake mzazi.


Baba yake Mourinho anayejulikana kwa jina la Felix amefariki nchini kwao Ureno akiwa na miaka 79, na kumuacha Mourinho akielezea majonzi yake kupitia Instagram.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram kocha huyo aliweka picha ya baba yake huku ikiwa na rangi nyeusi na nyeupe (B&W) na hakuandika kitu huku maoni ya mashabiki wakionekana kumpa pole.
Katika enzi za uhai wake mzee huyo wa Mourinho alikuwa akicheza mpira katika nafasi ya ugolikipa ambapo ashaidakia Ureno mara moja huku akiichezea Vitoria Setuba michezo 250.
Kilichomuua mzee huyo inadaiwa ni maradhi ya umri kwani alikuwa hakauki hospitali kila mara na sasa tukio zima la msiba wake litafanyika siku ya Jumanne.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Ads

Blog Archive