By Brown Mgeni
Wiki moja imepita tangu taarifa za staa wa zamani wa Man United anayeichezea Everton kwa sasa Morgan Scheinderlin kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Camille kuvuma mtandaoni, mastaa hao wameamua kuja hooney moon Tanzania.
Kupitia ukurasa wake wa instagram Scheinderlin amepost picha na kuthibitisha kuwa yupo Tanzania na mkewe Camille kwa ajili ya fungate yao mbugani, fursa ya watanzania kumuona itakuwa July 13 katika game dhidi ya Bingwa wa SportPesa Super Cup Gor Mahia na timu yake ya Everton uwanja wa Taifa Dar es salaam.
Kama utakuwa unakumbuka Morgan Scheinderlin ambaye ni raia wa Ufaransa si mwanasoka maarufu wakwanza kuwahi kufika Tanzania kutalii, katika kipindi hiki kifupi bali atakuwa wa tano baada ya David Beckham, Mamadou Sakho, Chris Eriksen na Victor Wanyama.
Scheinderlin anacheza nafasi ya kiungo mkabaji na alijiunga na Everton mwaka huu 2017 akitokea Man United, kwa mara ya kwanza Morgan Scheinderlin kuitwa timu ya taifa ya Ufaransa wakubwa ilikuwa 2014.
0 comments:
Post a Comment