Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe
amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga midomo na kusema kitendo
cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati wakifanya kazi yao
si sawa.
Freeman Mbowe
amesema hayo leo Alhamisi baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi
wa habari ambao walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa maelezo na kutakiwa kufika leo tena.
Mhe Edward Lowassa alipata wito
kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao
Makuu ya Jeshi la Polisi siku ya Jumanne tarehe 27 kufuatia kauli zake
alizozitoa ambazo zinasemakana kuwa ni uchohezi
Lowassa juzi alifika Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha
baada ya hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi
ya tarehe 29 Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo
lake haujakamilika hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.
0 comments:
Post a Comment