Huku Beyonce akiwa amejifungua salama na kukaa hospitalini kwa muda wa
wiki moja na nusu, hatimaye mwanamama huyo na watoto wake mapacha, wa
kiume na kike wameruhusiwa kutoka hospitalini.
Mjengo wenyewe
Habari zaidi kutoka katika ardhi ya US
inatutonya kwamba baada ya watatu hao kuruhusiwa kutoka hospitalini,
mumewe, Jay Z alikwishaandaa mjengo wa kupanga wa maana uliopo Malibu
ambapo watatakiwa kulipia dola 400,000 (zaidi ya milioni 900) kwa mwezi
tu.
Mjengo huo wa maana upo karibu na
Bahari ya Pasifiki ambapo watapata muda wa kuangalia meli na watu wakila
bata lakini pia mjengo una uwanja mdogo wa ndege. Mjengo una hekari
6.3, si hiyo tu, bado mtu mzima Jay Z anaendelea kusaka mjengo mwingine
wa kununua huko L.A (Los Angeles).
0 comments:
Post a Comment