Okwi akiikanyaga aridhi ya Dar es Salaam kwa madoido.
KLABU ya Simba, imetangaza rasmi kuwa, kesho Jumamosi itampokea straika wao wa zamani, Emmanuel Okwi, tayari kwa kumpa mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia timu hiyo.
Okwi, raia wa Uganda, ambaye aliwahi
kuitumikia Simba kwa vipindi viwili tofauti, anajiunga tena na timu hiyo
akitoke SC Villa ya nyumbani kwao ambayo alikuwa akiichezea mara baada
ya kuachana na SonderjyskE ya Denmark.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zacharia Hans Poppe, hivi karibuni alikuwa jijini Kampala, Uganda
kwa shughuli zake binafsi ambapo alitumia mwanya huo kumalizana na
Okwi.
Hans Poppe amesema: “Nilienda Kampala
katika mkutano wa mambo tofauti na soka, nikiwa kule nikaona mtandaoni
kuna picha inasambaa kwamba eti Okwi ameingia Dar, picha hiyo
ilimuonyesha akiwa amevaa kofia, sasa wakati naiona ile picha nilikuwa
karibu na Okwi, nikaona bora niwaumbue watu waongo, tukapiga picha,
nikazituma.
“Sasa watu wakabadilisha mada, wakaanza
kuzungumza kwamba tushamalizana naye wakati mimi nilitupia picha tu
bila ya kuandika chochote.
“Lakini hata hivyo, nikiwa kule
nimezungumza naye na tumekubaliana, hivyo atakuja hapa Jumamosi (kesho)
kusaini mkataba wa miaka miwili, tumeamua kumrudisha Okwi kwa sababu ni
mchezaji mzuri na mara kadhaa alikuwa akitupatia matokeo mazuri.
“Okwi ana uwezo wa kubadilisha matokeo
muda wowote, tumekuwa tukimfuatilia tangu awe anacheza soka Uganda na
tumeona bado ni mchezaji mzuri, kitendo cha kufunga mabao saba kwenye
mechi saba kimedhihirisha hilo.”
0 comments:
Post a Comment