Mwanaume mmoja nchini Msumbiji, Irmao do
Jovem amelazimika kulipa mahari ya mke wake aliyefariki kutokana na
matatizo ya kujifungua.
Kijana huyo amelazimika kulipa mahali
baada ya ndugu wa marehemu mke wake kumlazimisha kulipa ”Lobolo” kwa
kutishia kwamba la sivyo hatozikwa.
Hali hiyo imetokana na kijana huyo
kushindwa majukumu yake ikiwemo kutambulishwa kwa jamaa na ndugu za
mwanamke huyo kabla ya janga hilo kutokea, hivyo ili kuhakikisha kuwa
mazishi hayo yanafanyika, kijana huyo alilazimika kumnunulia nguo na
viatu mkewe aliyefarik.
Pia kukubali kulipa zaidi ya dola 800 na
kufanya harusi, ambapo familia ya kijana huyo imekubali kulipa lakini
pia imeshutumu tabia ya marehemu huyo, ameeleza ndugu wa kijana huyo
Irmao do Jovem.
”Tulijaribu kuchangisha fedha
walizotaka, lakini tuliweza kuchangisha dola 178 pekee.Hivyobasi ilibidi
kuweka ahadi ya kulipa fedha zilizosalia siku ya harusi”.
0 comments:
Post a Comment