Kumekua na taarifa zinatembea
mitandaoni na utani pia wa Mkuu wa idara ya habari kwenye club ya Simba
Haji Manara kwamba baada ya Emmanuel Okwi kuvunja mkataba na timu
aliyokua anaichezea huko Denmark, anarudi Simba na kocha akiamua
atacheza February.
Sasa baada ya kuwepo kwa hizo taarifa, shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeongea yafuatayo "Swala
la usajili wa mtu mnaemtaja Okwi, Simba inaweza ikamsajili lakini
itamtunza tu ama kucheza mechi za kirafiki lakini kucheza ligi kuu au
kombe la FA haiwezekani";
"Kucheza
ligi kuu au kombe la FA kwa msimu huu December January mpaka May June
hachezi, kwenye mpira wa miguu ukikosa utaratibu, kanuni na sheria mpira
wa miguu hamna…. tutakua tunafanya mambo ya ovyo ovyo mwanzo mwisho" – TFF
"Utaratibu huo unaozungumzwa na
kanuni hiyo vipo Ulaya ambako kuna Treni za umeme na vitu tofauti, kule
ni Ulaya na hapa ni Afrika, hapa ni Tanzania…. anaeongoza mpira na
mwenye mpira wake Tanzania ni TFF"
0 comments:
Post a Comment