RAPA anayetamba na
ngoma ya ‘Wana Ndoto’ Kala Jeremiah amesema sakata la Faru John ambalo
limeteka hisia za watu wengi kwa sasa alipolisikia kwa mara ya kwanza,
mapigo yake ya moyo yalimdunda hadi akaogopa.
Akipiga stori na Over Ze Weeked Rapa huyo amesema amekuwa akisikia
kashfa mbalimbali za ufisadi kwa muda mrefu, lakini hili la Faru John
limekuwa la aina yake.
“Nimekuwa nikijaribu kufuatilia ishu hiyo kwa kina ajabu nakutana na
habari zisizo eleweka kila mtu anamaelezo yake, sakata la Faru John
linanifanya niamini uwepo wa sakata la Twiga waliyowahi kupandishwa
Ndege na kusafirishwa Ughaibuni kinyamela.
“Naendelea kujiuliza maswali ambayo sijui majibu yake nitayapata wapi,
miongoni mwa yale ninayo jiuliza ni je kuna Faru wangapi wanaokufa huko
katika mbuga za wanyama, na je kwanini kutoweka kwa Faru John kuibue
gumzo kiasi hicho, huyo Faru alikuwa na kitu gani kikubwa cha ajabu,
lakini kubwa kuliko vyote nimetaharuki baada ya kubaini kuwa kumbe
Wanyama huwa wanapewa Majina ya Binadamu.” Alisema Kala Jerimiah
0 comments:
Post a Comment