
Jioni ya January 16 2017 ripoti
kutoka Geita kanda ya ziwa zilithibitisha kwamba Waziri mkuu mstaafu
Edward Lowassa amekamatwa na Polisi akiwa anakwenda kwenye mkutano wa CHADEMA hukohuko Geita ambapo baada ya kusambaa kwa taarifa hizo na baadae kuachiwa, Polisi Geita imeyasema haya baada ya kuhojiwa na AMPLIFAYA YA CLAUDS..
1: ‘Hatukumkamata
Edward Lowassa bali tulikua tumemshikilia tu huyu bwana, na sababu
kubwa kabisa za kuwa nae ni swala zima la ulinzi na usalama’ – Kamanda wa Polisi Geita
2: ‘Usalama
wa aina gani…… ni usalama wa kwake yeye kama yeye lakini pia na jamii
inayomzunguka, hiyo ndio hoja kubwa iliyokua imejitokeza‘
3: ‘Polisi
haikuwa na taarifa yoyote ya Edward Lowassa kuelekea kwenye mkutano wa
CHADEMA, na wakato tumemshikilia tulikaa nae mpaka tulipomaliza
mahojiano yetu na ndipo tulipomruhusu akaendelea na safari yake‘
ndipo polisi wakadai kuwa mpaka wakati ule walipokuwa wakihojiwa tayari Mh. Lowassa alikuwa akashaachiliwa.
0 comments:
Post a Comment