Nahodha wa Chelsea John Terry
alitimuliwa uwanjani dakika ya 66, baada ya kupewa kadi nyekundu, ambayo
ndiyo yake ya kwanza tangu mwezi Oktoba wakati ambapo Chelsea
wamewanyuka Peterborough mabao 4-1.
Chelsea waliitawala mechi hiyo licha ya kukabiliwa na mashambulizi kadha kutoka kwa Peterborough.
Terry alipewa kadi nyekundi baada ya kumchezea vibaya mshambulizi Angol.
Kutimuliwa
kwa Terry ni pigo kwa Chelsea ambao wameonyesha mechi safi baada ya
kushindwa na Tottenham, ambacho ni kipigo chao cha kwanza kati ya mechi
11 walizocheza.
0 comments:
Post a Comment